Michezo

Siku zahesabika kwa Papic

Papic kukaa benchi

 

Siku zahesabika kwa kocha Papic kuendelea kukinoa kikosi cha Yanga. Uongozi wa klabu ya Ruvu Shooting umemruhusu kocha wa kikosi hicho FELIX MINZIRO kwenda kujiunga na klabu ya Yanga huko visiwani Zanzibar ambako timu ya hiyo inashiriki mashindano ya kombe la Mapinduzi.

Msemaji wa Ruvu Shooting amesema uongozi wa Yanga umemtaka kocha huyo kwenda kukinoa kikosi cha Yanga huko Zanzibar hivyo tayari makubaliano yamefanyika na MINZIRO ameruhusiwa kwenda kujiunga na Yanga.

Kocha huyo anatarajia kuripoti kambini Yanga kesho.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents