Habari

Spika aamuru Mbunge Waitara atolewe nje ya Bunge

Spika wa Bunge, Job Ndugai ameamuru Mbunge wa Ukonga(CHADEMA), Mwita Waitara kutoka nje ya bunge hilo kwa kwa kosa la utovu wa nidhamu kwa kubishana na kiti cha Spika.

Spika Ndugai ameamuru Waitara kutoka nje ya bunge baada ya kuomba muongozo kufuatia kauli aliyotoa Spika wa Bunge kuwa wabunge wote wanaoikataa bajeti katika kuhitimishwa kwa bajeti ya 2017/2018 na upigaji wa kura ya wazi.

“Waitara sitaki miongozo, nakuomba ukae chini, Waitara nakupa onyo la kwanza, masanjeti wa bunge anzeni kukaa sawa, naomba askari ya bunge mkae sawa sawa popote pale mlipo, wewe unayeongea nakuomba utulie wenzako waongee, wewe Katibu anayenijibu ni nani? Ni huyo huyo Waitara?,” alihoji Spika Ndugai.

“Basi nakuomba Waitara utoke nje ya bunge sasa hivi kwa hiyari yako mwenyewe kabla sijaita wale mabwana wakubwa, nakuomba utoke nje haraka unanipotezea muda.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents