Michezo

Tetesi za Soka barani Ulaya Alhamisi, Neymar atafuta nyumba jijini Barcelona siku za kuwa PSG za hisabika, United kung’oa kifaa Crystal Palace

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar amekuwa akitafuta nyumba mjini Barcelona, licha ya tetesi kuibuka kuwa nyota huyo wa Kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 anajiandaa kurejea Nou Camp. (Sport)

Neymar shooting

Manchester United wamekubali kulipa ada ya pauni milioni 55 kumsajili mlinzi wa Crystal Palace, Aaron Wan-Bissaka, 21. (Record) Hata hivyo madai hayo yamekanushwa huku vilabu hivyo vikiendelea kushauriana kuhusu usajili wa kiungo huyo. (Mail)

Chelsea inapania kumuajiri kocha wa Derby Frank Lampard, kama maneja wake mpya kwa kandarasi ya miaka mitatu kufikia mwisho wa wiki hii. (Standard)

Bayern Munich wanajiandaa kujiunga na Manchester City katika kinyang’anyiro cha kumsaini kiungo wa kati wa Uhispania Rodri, 22, kutoka Atletico Madrid. (AS – in Spanish)

Kiungo wa kati wa Brazil Jorginho yuko tayari kuondoka Chelsea na kwenda kujiunga na Maurizio Sarri katika klabu ya Juventus mwaka mmoja baada ya kusajiliwa na Napoli kwa kama cha pauni milioni 50. (Mirror)

Inter Milan na Atletico Madrid wanataka kusajili beki wa England anaechezea klabu ya Southampton Ryan Bertrand, 29. (Mail)

Juventus wanaamini wataipiku Real Madrid katika usajili wa kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Mirror)Paul Pogba

Arsenal inapania kusaini beki wa Celtic raia wa Uskochi Kieran Tierney, 22, msimu ujao. (Mail)

Sporting Lisbon wanashauriana na Liverpool kuhusu usajili wa winga wa Ureno wa miaka 19, Rafael Camacho. (Standard)

Norwich wanamatumaini ya kumnunua beki wa England Max Aarons, 19, licha ya mchezaji huyo kunyatiwa na Manchester United. (Telegraph)

West Ham wameifahamisha Manchester United na Manchester City kuwa hawana mpango wa kumuuza nyota wa Kimataifa wa England anaecheza safu ya kati Declan Rice, 20, msimu huu wa joto. (Sky Sports)

Declan Rice

Arsenal wanajianda kuweka dau la kumnunua winga wa Red Bull Salzburg na Hungary Dominik Szoboszlai, 18. (Football Insider)

Kipa Tom Heaton amekataa ofa ya kandarasi mpya aliyopewa na Burnley.

Kipa huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 33 ataingia mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake wa sasa katika uwanja waTurf Moor mwezi ujao. (Guardian)

Tetesi Bora Jumatano

Paris St-German wako tayari kumuuza mshambuliaji nyota wa Brazil, Neymar mwenye umri wa miaka 27 msimu huu. (ESPN)

Real Madrid huenda wakamjumuisha kiungo wa kati Mbrazil Casemiro, 27, kwa ofa yoyote ya kusaini Neymar kutoka PSG. (Marca)Neymar

Manchester United wanataka Paul Pogba asiondoka katika klabu hiyo lakini akubali kuwa hali inaweza kubadilika waamue kumuuza nyota huyo wa Kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 . (Sky Sports)

Huku hayo yakijiri Real Madrid, wameonywa na rais wao wa zamani, Ramon Calderon kutomsajili Pogba. (Sun)

Manchester United watalazimika kulipa hadi pauni milioni 75 wakitaka kumsajili mlinzi Mfaransa Issa Diop,22 kutoka West Ham, baada ya Red Devils kukataa pendekezo la Hammer la kubadilishana wachezaji katika mkataba utakao mhusisha mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 23. (Mirror)Anthony Martial

Everton wanakaribia kukamilisha mchakato wa kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Andre Gomes, 25, kutoka Barcelona kwa pauni milioni 22. (Mail)

Ajenti wa Gareth Bale amepuuziliambali madai kuwa mshambuliaji huyo wa Real Madrid wa miaka 29 huenda akahamia Bayern Munich kwa mkopo. (Mirror)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents