Michezo

TFF yatangaza rasmi tarehe ya kupigwa mechi ya Simba SC na Yanga SC

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kupitia Mtendaji Mkuu wa bodi hiyo Bw. Boniface Wambura hii leo imetangaza rasmi tarehe itakazo zikutanisha klabu kongwe na hasimu Simba SC na Yanga SC.

Wambura ametangaza rasmi kuwa Simba SC na Yanga SC watacheza mchezo wao wa ligi kuu tarehe 29 mwezi wan ne mwaka huu.

Mbali na mechi hiyo kubwa na inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka hapa nchini michezo mingine ambayo imetolewa ratiba yake rasmi, klabu ya Simba imepangwa kucheza na Njombe Mji April 3.

Klabu ya Mtibwa Sugar dhidi ya Simba itakuwa Aprili 9 wakati Lipuli FC dhidi ya Simba Aprili 20.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents