Burudani

Tiwa Savage athibitisha kolabo na Sauti Soul kutoka mwaka huu

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, Tiwa Savage amethibitisha ujio wa kolabo yake na kundi la muziki kutoka nchini Kenya, Sauti Soul.

Muimbaji huyo ambaye kwa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sugarcane’, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe mfupi ambao umeweka wazi kuhusu ujio wa kolabo hiyo.

Too early in the year or na 😜 Massive African Collabo coming soon #GirlNextDoor @sautisol ft @tiwasavage  2018 gonna be SAVAGE trust me

Utakumbuka December 28 Sauti Soul nao walifanya hivyo katika mtandao wao wa twitter kuweka wazi ujio wa kolabo hiyo; “If you can’t wait for the Tiwa collabo just tweet #AfrikanSauce” waliandika Sauti Soul.

Kolabo hiyo itakuwa ni ngoma nyingi kwa Sauti Soul kufanya na msanii wa Nigeria ambapo kwa sasa wanafanya vizuri na ngoma ‘Melanin’ ambayo wamemshirikisha Patoranking.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents