Burudani

TPain awasili Dar

 

Msanii Faheem Rasheem Najm ambaye anajulikana zaidi kama T Pain jana usiku aliwasili jijini Dar-Es-Salaam tayari kabisa kwa ajili ya kupiga shoo kali katika str8 Music festival intercollege special 2010.

Msanii huyo ambaye ni mzaliwa Talahassee mjini Marekani, alitokea moja kwa moja kutoka Atlanta na kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius kambarage Nyerere majira ya saa nane kasoro akitokea nchini Afrika kusini ambako alipitia akiunganisha kuja Tanzania.

Msanii huyo anayejulikana zaidi kwa collabo zake na wakubwa wa muzikiĀ  na hasa sauti yake kali ambayo watu wengi wanasema anapenda matumizi ya autotune, anatarajiwa kufanya makamuzi pamoja na wasanii wenzake Gyptian, Mims na Elephant Man katika shoo ya ukweli kabisa ya Str8 Muzik Festival.

Show hiyo itafanyika leo katika viwanja vya Posta sayansi kuanzia majira ya saa Mbili za usiku na inategemewa kunogeshwa na wasanii kutoka nyumbani, baadhi yao kama Mangwea, Cpwaa na Sheta.

Bongo5 itakuwa sambamba nawe kuporomosha yatakayojiri.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents