Trump asema hajutii kutoa hotuba iliyozua ghasia katika jumba la bunge (+ Video)

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba hotuba yake ya wiki iliopita alipowataka wafuasi wake kuvamia bunge la Congress ‘ilistahili’.

Bwana Trump alisema kwamba ni upuuzi kwa wanachama wa Democrarts kuweka juhudi za kumshataki bungeni kwa ‘kuchochea uasi’.

Anaondoka afisini tarehe 20 Januari wakati ambapo rais mteule Joe Biden ataapishwa.

Bunge la uwakilishi linatarajiwa kupigia kura kifungu cha sheria kuhusu kumshtaki rais huyo siku ya Jumtano.

”Nadhani mchakato huo wa kunishtaki unasababisha hatari kubwa kwa taifa letu na unasababisha hasira kubwa . Sitaki ghasia” , bwana Trump alisema.

Alikuwa akizungumza alipokuwa akiondoka katika Ikulu ya Whitehouse kuelekea jimbo la Texas ili kuchunguza sehemu moja ya Ukuta uliojengwa katika mpaka wa taifa hilo na Mexico.

Ilikuwa mara ya kwanza kwa yeye kuonekana hadharani tangu ghasia za Capitol ambapo takriban watu watano walifariki na makumi kujeruhiwa ikiwemo maafisa wa polisi 60.

Wakati wa hotuba yake iliotolewa katika mkutano wa hadhara katika mji wa Washington tarehe 6 mwezi Januari , bwana Trump alirejelea madai yake yasio na ushahdi kuhusu wizi wa kura wakati wa uchaguzi wa urais wa Novemba 3 na kuwataka wafuasi wake kuvamia bunge

”Tutaenda katika jumba la bunge ili kuwapongeza maseneta na wabunge wetu kwa ujasiri wao na huenda baadhi yao hatutawapongeza sana , kwasababu huwezi kulirudishu nyuma taifa letu kwa udhaifu. Lazima uonyeshe uwezo wako” aliwahutubia maelefu ya wafuasi wake .

Alisema kwamba makamu wa rais Mike Pence ni sharti awe na ujasiri wa kufanya anachoweza kufanya , akidai bila msingi kwamba bwana Pence alikuwa na uwezo wa kikatiba kubadilisha matokeo ambayo yalikuwa yakihesabiwa bungeni siku hiyo.

”Najua kwamba kila mtu hapa ataelekea katika jumba la bunge ili kuhakikisha kuwa sauti zetu zinasikika kwa njia ya amani , alisema Trump.

Makumi ya watu wamekamatwa kuhusiana na ghasia hizo za wiki iliopita . Kati ya watu watano waliopoteza maisha yao , mmoja alikua afisa wa polisi huku mmoja akiwa mwandamanaji aliyepigwa risasi na polisi.

 

Wakati huohuo mbunge wa tatu,amesema kwamba ameambukizwa corona baada ya kujificha na watu waliokuwa hawajavalia barakoa katika chumba kimoja wakati wa ghasia hizo za januari 6.

Bunge la uwakilishi litapiga kura siku ya Jumanne kumuuliza makamu wa rais Mike Pence kutumia kifungu cha sheria cha 25 kumuondoa rais Trump kutoka afisini – wazo ambalo bwana Pence anadaiwa kupinga.

Kura hiyo inatarajiwa kugonga mwamba hivyobasi bunge baadaye litafikiria kutafuta kifungu cha kumshtaki rais Trump kwa ‘kuchochea uasi’.

Democrats wana idadi kubwa ya wabunge katika bunge la uwakilishi , hivyobasi mashtaka hayo huenda yakaungwa mkono kupitia kura .

Iwapo Kura hiyo itapita , rais Trump atakuwa rais wa kwanza nchini Marekani kushtakiwa mara mbili.

Hatahivyo, kushtakiwa kwake kutasababisha kuondolewa madarakani iwapo thuluthi mbili ya maseneta wataunga mkono kura ya maoni dhidi yake.

Hatua hiyo itahitaji idadi kubwa ya wabunge ya Republican na kufikia sasa , ni wachache walioonesha hamu ya kupiga kura dhidi ya rais kutoka kwa chama chao wenyewe.

Akizungumza kuhusu ziara yake katika jimbo la Texas , bwana Trump alipuuzilia mbali tishio la kumuondoa madarakani kikatiba.

”Kifungu cha sheria cha 25 katika katiba hakihatarishi kivyovyote uongozi wangu lakini kitakuja kumuandamana Joe Biden na utawala wa Joe Biden”, alisema.

Kulingana na gazeti la The New York Times , kiongozi wa bunge la Seneti kutoka chama cha Republican Mitch McConnell amewaambia wandani wake kwamba anafurahi kwamba Democrats wanataka kumshtaki rais Trump.

Seneta huyo wa Kentucky anaamini kwamba adhabu hiyo itarahisisha kumuondoa Trump katika chama cha Republican , lilisema gazeti hilo.

Bwana McConnell pia amewaambiwa washirika wake kwamba anaamini rais huyo alifanya makosa ambayo yalihitaji kuwasilishwa bungeni , lilisema gazeti la Washington Post.

Hatahivyo McConnell na kiranja wa wabunge wa Republican Kevin McCarthy, hawana mpango wa kuwashawishi wenzao kuunga mkono ama kupinga kura hiyo ya kutokuwa na imani dhidi ya rais Trump , kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Bofya hapa chini.

https://www.instagram.com/tv/CJ-uK32hsG3/

https://www.instagram.com/tv/CJ-uK32hsG3/

Related Articles

Back to top button
Close