Michezo

Tulitawala mchezo licha ya kupoteza dhidi ya Chelsea – Mourinho

Ligi kuu nchini Uingereza iliendelea usiku wa jana kwa miamba kadhaa ya soka kujitupa katika viwanja mbalimbali.

Huko Stamford Bridge mabingwa watetezi klabu ya Chelsea ilikuwa nyumbani kuwakaribisha Manchester United na kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 1-0.

Katika mchezo huo Alvaro Morata aliibuka shujaa baada ya kuipatia timu yake ya Chelsea bao kwa njia ya kichwa ambalo lililoamua matokeo hayo ya ushindi wa 1-0.

Baada ya mchezo huo kumalizika meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amesema timu zote mbili ziliweza kutawala mchezo na bahati haikuwa upande wao.

“Tuliweza kutawala mchezo na wao hivyo hivyo waliutawala.” Amesema meneja wa United,Jose Mourinho:

Mourinho ameongezaTulipata nafasi nyingi kama wao walivyopata, tuliamua kubadili muelekeo wetu wa mchezo na kutengeneza nafasi nyingi zaidi lakini hatukufanikiwa kupata goli.”

“Bado tuna michezo mingi ninaimani tutafanya vizuri hasa msimu huu tupo katika kiwango cha juu sana tunao Paul Pogba, Ibrahimovic na kurejea kwa Marcos Rojo.”

Kwa upande wa meneja wa Chelsea, Antonio Conte amesema anajiskia furaha kufanikiwa kuchomoza na ushindi mbele ya timu bora.

“Ninafuraha timu yangu kufanikiwa kuchomoza na ushindi mbele ya timu bora kama Manchester United,”amesema Conte.

Antonio Conte ameongezaKwa kuwa na ubora kama huu na jitihada za namna hii kwa hakika najiskia furaha na tutalazimika kuendelea hivi ni lazima tupambanie kwa kitu muhimu.”

 

Wachezaji wa Chelsea: Courtois (7), Azpilicueta (8), Christensen (6), Cahill (7), Zappacosta (6), Bakayoko (6), Fabregas (8), Alonso (6), Kante (7), Morata (8), Hazard (7)

Wachezaji wa hakiba: Willian (6), Drinkwater (6), Rudiger (6)

Kwa upande wa Manchester United: De Gea (7), Bailly (6), Valencia (6), Jones (6), Smalling (6), Young (6), Herrera (6), Matic (6), Mkhitaryan (6), Lukaku (6), Rashford (6).

Wa hakiba: Fellaini (6), Martial (6)

Mchezaji bora wa mchezo huo (Man of the match) alikuwa Cesc Fabregas

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents