Burudani

Tunda amtaka Matonya akubali kuwa yeye ndiye aliyemwandikia wimbo wa ‘Vaileti’

Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Tunda Man amemtaka Matonya kukubali kuwa yeye ndiye aliyemwandikia wimbo wa Vaileti ili tofauti zao za muda mrefu zimalizike.
Tundaman

Waimbaji hao ambao mwaka 2015 walipatanishwa na kituo kimoja cha radio na kudai wataigia studio kuandaa wimbo wa pamoja, bado wanaendelea kutupiana maneno.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumatano hii, Tunda alisema kuwa Matonya anatakiwa akubali ili mambo yaishe.

“Kila kitu ye anakijua, ndio maana mi nasema yeye ndo ana-create hadi hivi vitu vinatokea ugomvi, yeye ndo anataka viwepo, anajua kila kitu kuhusu Vaileti, anachotakiwa kufanya ni kuwaambia tu wananchi kuwa alichosema Tunda kuwa Tunda alifanya hii ngoma, aliandika mimi nimeimba lakini ilitakiwa na yeye aimbe lakini alishindwa kwa hiyo nikaimba mimi ngoma yote”, alisema Tunda man.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents