Siasa

Uchaguzi Uganda : Raia wakishiriki katika zoezi la kihistoria la upigaji kura

Raia wa Uganda hii leo wanapiga kura kumchagua rais na wawakilishi wapya wa bunge . Akizungumza siku ya Jumatano mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo jaji Simon Byabakama aliserma kwamba wapiga kura wa kiume ni zaidi ya milioni tisa huku wenzao wa jiniai ya kike wakiwa zaidi ya milioni tisa.

Katika uchaguzi huo rais Yoweri Museveni ambaye anatetea wadhfa wake anakabilia na upinzani mkali kutoka kwa mwanamuziki wa zamani maarufu Bobi Wine.

Bobi Wine ni mgombea ambaye amevutia idadai kubwa ya vijana nchini humo.

Rais Museveni anagombea muhula wa sita baada ya kuwa madarakani kwa miaka 35.

Hatahhivyo rais Museveni anajivunia utawala wake wa muda mrefu ambapo amefanya baadhi ya maenedeleo.

Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, anasema kuwa anawakilisha kizazi kipya cha vijana wa nchini humo, huku Yoweri Museveni, 76, akisema kuwa anasimamia ustawi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents