Bongo5 Makala

Uchambuzi: Nyimbo za Tanzania zenye beat kali zaidi mwaka 2013

Bila producer kutengeneza beat, hakuna msanii anayeweza kuwa na wimbo. Watayarishaji wa muziki wana mchango mkubwa zaidi katika mchakato wa utengenezaji wa nyimbo. Pamoja na kuwa na mchango huo mkubwa, wakati mwingine hushindwa kupata sifa wanazostahili na pongezi nyingi kuwaendea wanamuziki zaidi.

Kwakuwa mimi nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu kazi za maproducer wengi, nimeamua kuutambua mchango wao kwa kuandaa orodha hii ya nyimbo za mwaka 2013 ninazoona kuwa na beat kali zaidi. Nimefanya uchambuzi wa kawaida tu na sio wa kitaalam zaidi kama lugha ya utayarishaji muziki inavyotaka ili kila mtu aweze kunielewa zaidi.

Japo kuna nyimbo nyingi za mwaka 2013 zenye beat kali kutokana na mtazamo wa kila mmoja, kwangu hizi ndizo nyimbo zenye mdundo mkali zaidi na kama msomaji wa uchambuzi huu unaweza pia kuwa na maoni na uchambuzi tofauti na wangu.

Jikubali – Bel Pol – Produced by Lucci

Jikubali kwangu ni beat bora zaidi kwa ujumla wa beat zote zilizotengenezwa mwaka 2013 na ni beat ya pili kati ya zile zilizotengenezwa na Lucci kuipenda baada ya Problem ya Cpwaa. Ni beat ambayo tangu naisikia mara ya kwanza na hata leo nikiisikia nahisi bado ni mpya. Kwa Ben Pol hii ni beat kali mno kuwahi kutengenezewa.

Naipenda sana sauti ya organ yenye string inayotembea kwenye mzunguko wote wa beat. Usikiliza kwa makini hasa kwenye headphones utasikia kuna sauti za chekeche zilizokuwa ‘panned’ kwenye sikio moja na zinasikika kama vile zilichezwa live.

Nimependa pia matumizi ya kick inayopiga zaidi kama ngoma nzito na kubwa zinazotumika na wacheza ngoma wa Kisukuma. Ninakuja kuguswa zaidi na ‘distorted guitar’ linalochalazwa mwishoni na kuiachia piano inayoumaliza wimbo.

Kama Zamani – Mwana FA– Produced by P-Funk, instrumentals by Kilimanjaro Band

Leta beat zote za hip hop zilizotengenezwa mwaka huu, Kama Zamani kwangu ni beat bora zaidi kwasababu nyingi. Sababu moja kubwa ni beat ya hip hop iliyotengenezwa na bendi. Sio bendi tu, ni Kilimanjaro Band aka Wana Njenje.
Kwa mchanganyiko huo tayari Umetengeneza ukongwe ndani ya kitu kipya sawa na kuchanganya mnyinyo wa siku nyingi na wa sasa na kuzalisha ladha ya aina yake. Kama lilivyokuwa wazo lake mwenyewe, kutengeneza wimbo wenye wa hip hop wenye fusion ya nyimbo mbalimbali hususan Jazz, ilimchukua miezi kadhaa kuumaliza wimbo huu kwa kushiriki kwenye mazoezi ili kupata kitu bora.

http://www.youtube.com/watch?v=I01yby6VmTg

Come Over – Vanessa Mdee – Produced by Nah Reel & Erasto Mashine

Najua kuna baadhi wanaoweza kuhoji kuwa huu ni wimbo mpya mno pengine kuwa kwenye orodha hii lakini hiyo haijanizuia kuipa heshima yake kazi hii maridadi. Napenda mno jinsi beat inavyoanza hasa kwakuwa kutanguliwa milio maarufu kwenye nyimbo za techno hasa zile za zamani kidogo. Nimependa jinsi Nah Reel alivyocheza drums kwenye beat hii na jinsi ambavyo amezibadilisha badilisha. Producer ametengeneza fusion ya aina yake hasa kwakuwa unaweza kusikia Uafrika mwingi kwenye wimbo kwa kutumia sauti za marimba.

Lava Lava – Shaa – beat produced by Giggz, MJ Records

Nilikuwa sijawahi kuujua ukubwa wa wimbo huu hadi pale nilipomshuhudia Shaa akiuperform live wimbo huu kwenye fashion show ya Fashion Avenue iliyoandaliwa na Ally Rehmtullah kwenye hoteli ya Serena. Kwenye wimbo huu huna vingoma vinavyocheza kwenye spika zote kwa kupokezana zinazosikika kwa uzuri zaidi ukivaa headphone na vinavutia sana. Pia huna mlio wa sauti za synthesizer inayotembea ndani ya verse imepigwa kwa ustadi sana huku ikisambaa kwenye masikio na inaskika vizuri zaidi pale ambapo drums zinanyamaza.

Nje ya Box – Joh Makini & Nikki wa Pili ft G-Nako – Produced by Nah Reel/Chizan Brain

Niseme kuwa napenda kila nachokisikia kwenye beat ya wimbo huu. Nimependa jinsi ambavyo Nah Reel ametumia piano kwenye beat ya hip hop, sauti ambazo zimepewa shavu zuri na sauti za synch zinazosikika vizuri zaidi wakati wa chorus.

Kumbe – Peter Msechu Ft. Joh Makini – Produced by Fundi Samweli

Ni beat inayoendana zaidi na uimbaji wa Msechu. Inasikika ikiwa imepigwa live zaidi kuanzia piano, gitaa na gitaa ya bass. Ile chakacha inayosikika inaufanya wimbo usikike kiafrika zaidi. Ni beat ambayo ukiivulisha sauti zote bado utaendela kuiskiliza na ukaipenda. Piano zimepigwa kiustadi mkubwa na kupewa support na sauti za string.

Sio mimi – Madee – Produced by Marco Chali

Kwa mwaka 2013 hakuna wimbo unaoweza kuchezwa club na ukapata shangwe kama Sio Mimi. Ni beat kali itakayokulazimisha tu ucheze ama ukitikise kichwa kila unapousikia. Ni miongoni mwa beat kali zaidi kutoka MJ Records mwaka huu.

Tupogo – Ommy Dimpoz ft J-Martins – Produced by Man Walter & Marco Chali

Tupogo ni miongoni mwa zile beat safi na zilizofanyiwa mixing nzuri. Kwangu mimi, Tupogo ndio wimbo wenye baseline kali zaidi na iliyoutawala zaidi wimbo. Nyimbo zinazoimbishwa na baseline ni chache na kama producer akifanikiwa kufanya hivyo, wimbo hutambulika mapema hata kama ukipigwa kwa mbali hasa kwenye spika kubwa kwakuwa base itakuwa ikisikika zaidi kuliko vitu vingine.

Saxophone iliyocharazwa pia imeipa ‘ukubwa’ wimbo na kuufanya huu uwe tofauti na nyingi za aina yake.

Promise – Shaa – Produced by Manecky

Promise ni wimbo wa tatu wa Shaa kwenye list hii. Ukitaka kunielewa vizuri kwa nini beat ya wimbo huu ni kali ni lazima uwe umewahi kusikiliza nyimbo nyingi zaidi ya zile zouk halisi duniani ambazo kama wewe ni mtazamaji mzuri wa Trace TV Tropical unaweza kupata mfano halisi. Promise ni miongoni mwa nyimbo bora zaidi zilizotoka mwaka huu. Si tu kwa uandishi wa maneno mazuri ulifanywa na Barnaba pamoja na sauti tamu ya Shaa, bali pia ni ule utayarishaji wa ladha ya zouk halisi wa Manecky.

Monifere – Gosby ft Vanessa & Jux – Produced by Randy & B’Hits

Beat ya Monifere imetengenezwa na producer wa Kenya aitwaye Randy. Ni beat kali mno ambayo kama ukiisikia kwa mara ya kwanza huchelewi kuhisi imetengenezwa Nigeria au nchi za Afrika Magharibi. Sehemu ninayoipenda zaidi beat ya wimbo huu ni pale mwishoni ambako huwa napenda nipaloop kupata uhondo zaidi.

Jana na Leo – Young Killer & Stamina ft Quick Rocka – Produced by Deey Classic & Mona G

Beat ya wimbo huu imetengenezwa na Deey Classic (producer wa Mwanza aliyetengeneza wimbo wa Kala Jeremiah, Dear God). Katika wimbo huu nimependa zaidi ule utulivu wa organ inayotambaa kwa kusambaa masikioni.

Sio Kama wale – Banana Zorro

Beat ya ‘Sio Kama Wale’ ni zile ambazo huwezi kuzisikia mara kwa mara kwenye muziki wa Tanzania hasa kwakuwa ni wimbo unaOihitaji kupigwa na bendi na watu wanaojua muziki. Ni beat nzuri ya kusikiliza wakati wa lunch ama wakati unapenda kutafakari mambo. Ni muziki mzuri unaoOnesha ukomavu pia wa muziki wa Tanzania hasa kwa kuchanganya nyimbo zenye ladha za jazz na ile saxophone ya ukweli.

Watch Me – Country Boy – produced by Mesen Selekta

Mesen Selekta ni kati ya maproducer wachache viraka nchini. Anazo sifa zinazofanana pia na Pancho kwa maana ya uwezo wa kutengeneza beat za aina nyingi. Alichokifanya kwenye beat ya Watch Me, kimenifanya nimkubali zaidi. Ninachopenda kwenye beat hii ni lile gitaa lenye basi linalotembea zaidi kwenye beat nzima na jinsi alivyocheza na effects.

My Number One – Diamond – produced by Sheddy Clever

Kwa wengi My Number One unaweza kuwa ndio wimbo wao bora wa mwaka. Beat ya wimbo wake imetayarishwa na producer mdogo kiumri, Sheddy Clever. Ninaipenda zaidi ile saxophone iliyocharazwa vizuri ndani pamoja na lile gitaa linacheza kama nyimbo za Afrika Kusini. Hata hivyo kwangu mimi Number One si beat namba moja kwa mwaka huu.

Richie Mavoko – Roho Yangu – Mazuu Records

Roho Yangu ilifanikiwa kuhit kwa muda mfupi tu tangu itoke na kwangu mimi sauti za Rich ndizo zilizobeba zaidi utamu wa wimbo. Pamoja na kuwa beat nzuri, naiona beat ya wimbo huu kuwa haina kitu cha kushtua sana.
Sugua Gaga – Shaa – produced by Shirko

Nimeanza kumfuatilia Shriko tangu alipowatoa 2 Berry na wimbo wao wa kwanza ‘Na Wewe Tu’ na tangu hapo akawa miongoni mwa watayarishaji wa muziki ninaowaheshimu sana.

Amekuja kunifurahisha zaidi kwenye Sugua Gaga. Sugua Gaga ina beat kali na ni miongoni mwa zile beat zinazoweza kutoa jibu la kuridhisha la wale wanaotafuta kujua nyimbo za Kitanzania zinatakiwa kuwa na ladha gani.

BMS – Gosby – produced by Pancho

Nilipoisikia beat ya BMS, nilizidi kujustify mtazamo wangu kuwa Pancho Latino ni miongoni mwa maproducer watano wakali zaidi Tanzania. Kwa wanaomfahamu Pancho vizuri watakuwa wanatambua kuwa hakuna wimbo asioweza kuutengeneza. Kuanzia mnanda, mchiriku, hip hop, zouk, dancehall na kila aina ya nyimbo. Hivyo kwa kutengeneza beat ya BMS ambayo kwa Marekani beat kama hizi zinafanywa zaidi na watu kama Bryan-Michael Cox, Sean Garrett ama Rico Love, nimempa salute Pancho.

Love Me – Izzo B ft Shaa & Barnaba – produced by Nah Reel

Kama Nahreel asipotajwa kwenye kipengele cha maproducer bora wa mwaka 2013, nitaandamana. Love Me ina beat kali. Zile kick zinazound kama ngoma nzito zimeifanya isikike kama midundo anayoipenda T.I. Nimepende pia ile distorted guitar.

Wazo la leo – Stamina ft. Fid Q – produced by P-Funk

Kinachokamata zaidi beat ya ngoma hii ni ile baseline iliyotawala kote na kisha kwa mbali inapewa support na chords zinazofanana na za piano iliyoshushwa ambazo si rahisi kuzikia kwenye nyimbo za kibongo. Nimependa pia string zinazosikika kwenye chorus.

Beat zingine kwa kuzitaja tu ni Mdudu ya Solothang (Mesen Selekta), Latino Nation ya Dj Choka (Pancho), I Love You ya Cassim, Thanks God ya Godzilla (Marco Chali), Doro ya Walter Chilambo (Marco Chali), So Crazy ya Maua Sama ft Mwana FA (Marco Chali).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents