Burudani

Kajala achukizwa kuzushiwa anatembea na mume wa mtu ‘nimekwazwa sana’

Msanii wa filamu nchini Kajala Masanja amefunguka ya moyoni na kudai kuwa amechoshwa kuzushiwa anatembea na mume wa mmiliki wa blog ya mitindo nchini (8020 Fashions) Shamim Mwasha huku akidai kuwa si kweli.

Shamim na Kajala.
Shamim na Kajala

Kajala ameamua kukanusha tetesi hizo kupitia akaunti yake ya Instagram baada magazeti ya udaku kumtuhumu amekuwa akitembea na mume wa Shamim.

“Nadhani namjua huyu dada siku nyingi sana kabla ata ya wengine wenu kumjua tunaheshimiana sna na atujawahi kukoseana sasa sijui nani alie anzisha habari ya mimi natembea na mume wake na sijui alifanya ivyo kwa makusudi gani naumia kila siku kwaajiri ya ujinga wa watu na hayo magazeti nikiwaambia nipeni ushahidi wa kuwa natembea na mume wa shamim sijui kama mtafanya daah sijui nisemeni nini @8020fashions mpz enjoy ndoa yako acha na wapumbavu nimevumilia nimeona bora leo niandike unajua sipendagi kuongea lkn gazeti la jana limenikwaza sana,” aliandika Kajala.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents