Habari

Upepo waezua mapaa ya madarasa na nyumba za watu Morogoro

Zaidi ya nyumba 21 na madarasa matatu ya shule ya msingi Kalengakule zimeezuliwa na upepo uliombatana na Mvua na kusababisha wananchi kukosa makazi katika kata ya Kalengakule tarafa ya Mlimba wilaya Kilombero mkoani Morogoro.

Akizungumza na EATV kaimu afisa tarafa ya Mlimba Bwana Acley Mhenga amesema tukio Hilo limetokea disemba 31 mwaka 2021.

Mhenga anasema licha ya tukio Hilo kuharibu Mali lakin pia watu wawili wamejruhiwa baada ya kuangukiwa na nyumba ambapo ameiagiza kamati ya maafa ya eneo Hilo kuangalia namna ya kuwasaidia wananchi.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo Diwani wa kata ya Kalengakelu Martha Mkula ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wanyonge kuwatembelea wananchi wake ambapo ameomba hatua za haraka zichukuliwe ili kunusuru wananchi hao pamoja na ukarabati wa vyumba hivyo vya madarasa.

Chanzo Eatv.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents