Habari

Urusi kuongeza thamani ya biashara na Afrika, Rais Putin athibitisha hilo 

Rais Vlamidir Putin wa Uurusi amesema hapo jana kuwa kunauwezekano wa kuongeza maradufu thamani ya biashara kati ya Urusi na Afrika katika kipindi cha miaka minne au mitano inayokuja.

Image result for Vladimir Putin and African leader

Putin ametoa matamshi hayo wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa kilele wa siku mbili kati ya Urusi na Afrika unaofanyika kwenye mji wa mapumziko wa Sochi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Deutsche Welle, Biashara kati ya pande hizo mbili tayari imeongezeka maradufu katika kipindi cha maika mitano na kufikia thamani ya dola bilioni 20 za Marekani, kiwango ambacho Putin amekitaja kuwa kidogo.

Moscow ilikuwa na ushawishi mkubwa barani Afrika wakati wa enzi ya kisovieti kwa kuunga mkono juhudi za kutafuta uhuru pamoja na kutoa mafunzo kwa viongozi wa kiafrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents