Michezo

USAJILI: Liverpool yawinda saini ya Keita

Klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza ina husishwa kuwania saini ya kiungo wa Red Bull Leipzig, Naby Keita huku RB ikihitaji dau la pauni milioni 70 ili kumuachia mchezaji huyo.

Mchezaji wa klabu ya Red Bull Leipzig, Naby Keita

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Liverpool, Dietmar Johann Wolfgang “Didi” Hamann anaamini pauni milioni 70 siyo fedha nyingi mbele ya wenyeji hao wa Anfield kuinasa saini ya Keita ila hofu yake ni the Reds kuendelea kumuhitaji kwaajili ya mipango yake ya baadae.

Kiungo huyo wa Red Bull Leipzig amekuwa kwa muda mrefu akihushwa kuhamia Anfield na katika ligi ya Bundesliga ya nchini Ujerumani.

Keita raia wa Guinean mwenye umri wa miaka 22 msimu ulimalizika amefanikiwa kufunga magoli huku akichangia pasi zilizo sababisha magoli.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents