USAJILI: Utani wa Haji Manara kwa Yanga
Katika siku za hivi karibuni aliyekuwa Msemaji wa klabu ya Simba SC, Haji Manara ameonekana akitupia picha zake katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram huku zikiwa na maneno ya utata ambayo yanaonekana kama kuashiria jambo linaloendana na usajili wa ligi kuu msimu huu.
Siku chache toka klabu ya Yanga SC kumsajili mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha Simba, Ibrahim Ajib Migomba kumekuwa na minong’ono kwa wekundu hao wa msimbazi kulipiza kisasi kwa kumsajili mchezaji raia wa Rwanda Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima.
Aliyekuwa Msemaji wa klabu ya Simba SC, Haji Manara Haruna akiwa na mchezaji Hakizimana Niyonzima
Baada ya kupita siku chache toka aposti picha zake zenye ujumbe huo mapema hii leo Yanga SC imetoa taarifa ya kuachana na aliyekuwa mchezaji wake wa kimataifa raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima baada ya kushindwa kuafikiana.
Mchezaji wa klabu ya Yanga SC, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima
kupitia kwa Katibu Mkuu Boniface Mkwasa amesema Haruna Niyonzima bado ana mkataba mpaka mwezi Julai na Yanga Sc, lakini hawata weza kuendelea kuwa nae kwa msimu ujao kwakushindwa kuafikiana katika mazungumzo kati yao na mchezaji huyo licha ya timu hiyo kuwa na nia za kuendelea nae kwa misimu miwili ijayo.
Zifuatazo ni picha za Haji Manara zikiwa na ujumbe wa utata wa kuashiria jambo katika usajili wa klabu ya Simba SC
BY HAMZA FUMO