Habari

UTAFITI: Kiwango cha hatari kufa kwa mwenye ‘CORONA’ hutegemea Umri, afya na jinsia ya mtu

Utafiti wa sasa unadhani kuwa kati ya watu 40, watu watano wana virusi vya corona na watu 1,000 wanaoweza kufa kutokana na ugonjwa huo, asilimia moja ya watu 1000.

Wahudumu wawili wa afya ,wakiwa wamevalia mavazi ya kujikinga virusi vya corona wakijiandaa kwenda kuwatibu wagonjwa wa corona huko Wuhan, China.

Siku ya jumapili, Waziri wa afya Matt Hancock alisema kuwa serikali ya Uingereza watafanya uchunguzi vizuri na kuangalia idadi hiyo ya vifo kuwa chini ya asilimia mbili au chini ya hapo.

Ingawa huwa inategemea na sababu kadhaa kama umri, jinsia na hali ya afya ya mtu pamoja na mfumo wa afya uliopo sehemu husika.

Kuna ugumu gani kubaini idadi ya vifo vyake?

Katika kiwango cha elimu ya juu ni ngumu ubaini idadi ya watu wanaopoteza maisha kutokana na corona.

Hata kuhesabu visa vya ugonjwa huo ni ngumu pia. Kesi nyingi za ugonjwa huo huwa hazifahamiki kwa sababu watu wana tabia ya kutokwenda kwa daktari wanapopata dalili za ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Taarifa za vifo vinavyotokana na corona, zinazoripotiwa katika maeneo mbalimbali duniani inawezekana kuwa zimepangwa kwa kipindi cha muda fulani.Four people cross the road wearing medical masks in Beijing, China

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na chuo cha Imperial, zinasema kuwa mataifa mbalimbali yako kwenye nafasi nzuri au mbaya ya kubaini maambukizi hayo kwa kuwa ni ngumu kuhesabu visa vya ugonjwa huo.

Hivyo katika kesi ambazo zimeripotiwa ,inawawia rahisi kuongeza idadi ya vifo. Lakini unaweza kupata mtazamo ambao si sahihi kwa upande mwingine.

Huwa inachukua muda kwa matokeo ya maambukizi kuwa kifo.

Kama ukijumuisha kesi za maambukizi yote ambayo hayajapata nafasi ya kufanyiwa vipimo, unaweza kupunguza makadirio ya vifo kwa sababu ya maambukizi ambayo hayafahamiki na matoeo yake ni vifo hapo baadae.

Wanasayansi wamejumuisha ushaidi wa kila maswali ili kupata picha ya idadi ya vifo.

Kwa mfano, wamekadiria kesi za maambukizi yanayoweza kujitokeza kuanzia kwenye dalili za mwanzo kabisa, na kuangalia kundi la watu kwa karibu kama wasafiri wa anga.

Hali ya maambukizi

Lakini kuna majibu tofauti pia katika kila ushahidi, ambao unaweza kuongeza nafasi za kuonyesha picha halisi ya tatizo lililopo.

Kama utatumia takwimu za Hubei peke yake, eneo ambalo vifo vilivyosababishwa na corona vilikuwa juu zaidi ya maeneo mengine ya China, basi makadirio ya vifo yangekuwa mabaya zaidi.

Hivyo wanasayansi pia wameangalia namna nzuri ya kukadiria.

Ingawa njia iliyochaguliwa bado haiwezi kueleza ukweli wa idadi ya vifo vinavyosababishwa na corona.

Uko kwenye hatari gani ya uambukizwa?

Baadhi ya watu wako kwenye hatari ya kufa wakipata maambukizi ya virusi vya corona tofauti na wengine, kama vile wazee, wagonjwa na wanaume pia.

Katika utafiti wa kwanza uliojumuisha kesi 44,000 nchini China, idadi ya vifo ilikuwa kubwa mara kumi zaidi kwa wazee kuliko watu wenye umri wa kati.Presentational white space

Idadi ya vifo iko chini kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 30-kulikuwa na vifo nane katika kesi za wagonjwa 4,500.

Na vifo hivyo viliwatokea mara tano zaidi kwa watu ambao wana ugonjwa wa kisukari , ugonjwa wa moyo au wenye matatizo ya kupumua.

Kuna idadi kubwa ya vifo vya wanaume ukilinganisha na wanawake.

Sababu zote hizo ukizijumisha bado hatuwezi kupata picha kamili ya mtu ambaye yuko kwenye hatari katika kila eneo.Watu wapatao 621 wameambukizwa na virusi katika meli ya Diamond Princess huko JapanWatu wapatao 621 wameambukizwa na virusi katika meli ya Diamond Princess huko Japan

Watu wako kwenye hatari gani katika eneo walilopo?

Kundi la wazee wenye umri wa miaka 80 nchini China wanawezekana kuwa katika hatari tofauti na wazee wa umri huo katika maeneo ya Ulaya au Afrika.

Maambukizi haya kupona huwa yanategemea tiba ambayo mtu anaweza kupata.

Hivyo inategemea na upatikanaji wa huduma na hatua ambayo mgonjwa yuko nayo.

Kama utapona ugonjwa huu, basi mfumo wa afya unaweza kukabiliana na ugonjwa huu katika eneo husika.Royal Free Hospital in LondonMgonjwa wa Corona huko Uigereza , anahudumiwa katika hospitali ya madaktari mabingwa ya kifalme mjini London

Corona ni hatari zaidi ya mafua?

Hatuwezi kulinganisha idadi ya vifo kwa sababu watu wengi wenye dalili za mafua huwa hawaendi kumuona daktari.

Hivyo hatuwezi kusema watu wangapi wana mafua au wana virusi vipya.

Lakini mafua yanaendelea kuua watu nchini Uingereza haswa wakati wa kipindi cha baridi.

Takwimu hii inajumuisha wanasayansi kuonyesha picha ya uhalisia wa hatari ya mlipuko wa virusi vya Corona kuwasili Uingereza.

Lakini cha muhimu ni wafu kufuata ushauri uliotolewa na shirika la afya duniani kuwa watu wanapaswa kuosha mikono, kujizuia kuwa karibu na watu wanaokohoa na kupiga chafya na kujaribu kutoshika macho,pua na mdomo.

Jedwali

Mada zinazohusiana

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents