Michezo

Van Gaal: Bado tuna fursa ya kutinga nne bora

Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa harakati za timu yake kufuzu katika kombe la Vilabu bingwa Ulaya zingezimwa iwapo timu hiyo ingepoteza dhidi ya Manchester City,lakini sasa anaamini wana fursa kubwa ya kuwa katika timu nne bora.

3266314B00000578-0-image-a-53_1458502144456

Bao la ushindi Manchester United lilofungwa na Marcus dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester City siku ya jumapili.

Kikosi hicho cha Van Gaal sasa kiko nafasi ya sita lakini kiko pointi moja pekee nyuma ya Manchester City walio katika nafasi ya nne.

”Pengo lililopo lingeongezeka iwapo tungepata droo ama hata kupoteza,ingekuwa vigumu sana”,alisema mkufunzi huyo wa United.Sasa hatma yetu iko mikononi mwetu lakini lazima tuendelee kushinda”.

”Tuna mechi nyingi za nyumbani ukilinganisha na zile za ugenini na hatushindwi sana katika uwanja wa Old Trafford,kwa hivyo tuna fursa’

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents