BurudaniVideos

Vanessa Mdee aeleza ushauri aliopewa na Trey Songz na kosa ambalo wasanii wengi wa Bongo hulifanya

Vanessa Mdee alikuwa miongoni mwa wale wasanii ambao kwa mwaka hutoa wimbo mmoja tu. Sababu zake za kufanya hivyo ni kutokana na kuweka nguvu, muda na fedha nyingi kwenye wimbo mmoja ambao wakati mwingine uwekezaji wake huwa kama wa album.

Hata hivyo, desturi hiyo ilibadilika baada ya kukutana na Trey Songz mwaka jana aliyemueleza kuwa hilo ni kosa kubwa.

“Trey Songz alituambia kile amegundua na kazi zetu, akasema nguvu yako ipo kwenye kutoa content, the world is so fast, mtandaoni watu wanashika nyimbo kila siku, zinapokelewa na zinatupwa. Ukiwapa nafasi mashabiki kukusahau, unaweza pia ukapotea, so engage them hata kama sio kwa muziki all the time, but make sure that chochote kile unachokifanya kinauplift muziki,” Vanessa aliiambia Bongo5.

“In that moment nikapata jibu la maswali mengi niliyokuwa najiuliza na nikasema sitarudia tena and I am working on it effectively.”

Vee amedai kuwa kabla ya kutoa album yake Money Mondays mwezi March, ataachia ngoma mpya na video.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents