Burudani

Vanessa Mdee afanya kazi na hit maker wa ‘Duro’ Tekno wa Nigeria

Vanessa Mdee ni msanii ambaye hupenda kupika mambo makubwa kimya kimya bila kuoesha hata dalili mpaka anapokaribia kupakua ndio huweka wazi. Lakini safari hii amefanya tofauti kwa kutupa taarifa mapema tutarajie makubwa kutoka kwenye ziara yake ya Nigeria.

Vanessa and Tekno

Baada ya kushinda tuzo ya AFRIMA 2015, Jumapili iliyopita Lagos, Nigeria ameutumia vizuri muda wake aliokaa nchini humo kufanya kazi na wasanii na ma-producer wa Naija.

Baada ya kushare na mashabiki wake kuwa amerekodi wimbo wa hit maker wa ‘My Woman, My Everything’, Patoranking, pia kuna kazi nyingine aliyofanya na hit maker wa ‘Duro’ Tekno Miles ambaye pia ni producer.

Tekno alipost picha akiwa na Vee pesa na kuandika, “Get ready #Vee&Tek cc @vanessamdee”

Na Vanessa naye akapost picha hiyo hiyo na kuandika; “wait for it … @teknoofficial #Alhaji #MoneyOnTheTrack”

Baada ya kutoka Nigeria Vanessa ameenda Johannesburg, Afrika Kusini ambako anatarajia kutumbuiza kwenye tamasha la Africa Music Concert litakalofanyika Ijumaa ya leo November 20. Wasanii wengine watakaotumbuiza ni pamoja na Wizkid, Davido, AKA, Cassper Nyovest, Jose Chameleone, Victoria Kimani na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents