Burudani
Vanessa Mdee ajumuishwa kwenye album ya Reekado Bank ‘Spotlight’
Muimbaji wa Nigeria, Reekado Bank amemjumuisha Vanessa Mdee kwenye album yake, Spotlight.
Msanii huyo aliye chini ya label ya Don Jazzy, Mavin ameandika kwenye Instagram: Thanks for your contribution on the album V!! @vanessamdee #Tanzania #EastAfrica.”
Bank huyo Jumatano hii atakuwa na listening party ya album jijini Nairobi.
Spotlight itakuwa na nyimbo kama ‘Katapot’, ‘Sugar baby’, ‘Corner’, ‘Tomorrow’, ‘Oluwa ni’ , ‘Standard’ na zingine. Itakuwa na nyimbo 18.