Michezo

Vicent Kompany atangaza kuutetea ubingwa wao msimu ujao kama ilivyofanya United mwaka 2009

Haikuwa vibaya kwa beki wa klabu ya Manchester City, Vincent Kompany na wachezaji wenzake kuanza kusherehekea ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza hapo jana siku ya Jumapili kwakuwa hapana shaka sasa taji hilo ni lakwao.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola akionyesha shukrani kwa mashabiki wa Manchester City baada ya ushindi wao dhidi ya Tottenham

Guardiola anaamini kuwa wachezaji ni lazima watakuwa na furaha pale wanapoyaona mafanikio. Nahodha wa City, Vicent Kompany amesema kuwa sasa ni muda wa kuona kikosi chao kikisukwa na kuimarishwa ili kiweze kuwa timu ya kwanza iliyotetea ubingwa huo wa Uingereza msimu ujao tangu walivyowahi kufanya hivyo Manchester United mwaka 2009.

Safu ya kiungo wa kati ni miongoni mwa sehemu muhimu ambayo Manchester City italazimika kuifanyia kazi kama inahitaji kuutetea tena ubingwa huo kwa msimu ujao na jicho lao likimuangazi mchezaji wa Shakhtar Donetsk, Fred.

Wakati kwa nafasi ya winga yupo Raheem Sterling , Leroy Sane na Riyad Mahrez wa Leicester City ambaye anampango wa kuachana na timu hiyo.

Tangu Manchester City ilivyopata kutwaa taji la Uingereza kwa mara ya mwisho hizi ndiyo timu zilizofuata badala yake

  • 2013/2014 Manchester City (2014/2015 – 2nd)
  • 2014/2015 Chelsea (2015/2016 – 10th)
  • 2015/2016 Leicester City (2016/2017 – 12th)
  • 2016/2017 Chelsea (2017/2018 – currently 5th)
  • 2017/2018 Manchester City (?)

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents