Videos

Video: Melania Trump amtetea mumewe kufuatia shutuma za udhalilishaji wanawake

Melania Trump amemtetea mume wake, Donald Trump katika mahojiano ya kwanza tangu mgombea huyo wa Urais wa chama cha Republican ashutumiwe kuhusika kwenye vitendo vya udhalilishaji wa wanawake.

Ameziita shutuma hizo za uongo na kudai kuwa mumewe alikuwa kwenye mazungumzo ya kawaida ya wanaume kwenye mkanda wa mwaka 2005 ambao alisikika akizungumza maneno machafu kuhusu wanawake. Wanawake takriban 9 wamejitokeza hadharani wakidai kuwa Trump aliwafanyia udhalilishaji wa kimapenzi.

“Ninamuamini mume wangu,” Melanie alimwambia mtangazaji wa CNN, Anderson Cooper Jumatatu hii.

“Hili lilipangwa na upinzani. Na taarifa zenyewe, waliangalia historia ya wanawake hawa? Hawana taarifa zozote.”

Pia alisema kuwa hajawahi kumsikia mume wake akizungumza lugha chafu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents