Burudani

Video: Octopizzo aachia video ya wimbo aliomshirikisha staa wa Marekani, August Alsina

Rapper anayeiwakilisha Afrika Mashariki, Octoppizo kutoka Kenya ameachia rasmi video ya wimbo wake uliovuja mwaka jana “This Could Be Us”, ambao amemshirikisha mwimbaji wa R&B kutoka Marekani, August Alsina.

Habari mbaya kwa mashabiki waliokuwa na hamu ya kumuona August Alsina katika video hii ni kuwa, kwa bahati mbaya mtaisikia sauti yake tu kwasababu hajaonekana katika video.

Hii ni single ya tatu kutoka kwenye album ya pili ya Octopizzo iitwayo ‘Long Distance Paper Chasers (L.D.P.C)’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents