Burudani

Video: Penzi la Vera Sidika na Otile Brown linavyonogeshwa na mimba bandia

Kile kilichoonekana na wengi kama kiki sasa kimekua kwikwi, Otile na Vera Sika sasa wamekua gumzo mtaani na kwenye vyombo vya habari mahusiani yao yamechukua nafasi kubwa.

Mara tu walipoonekana pamoja wengi walidhania kuwa ni project ambayo inakuja na pengine Otile alihitaji uwepo wa Vera ili kuipa shavu project hii. Lakini kwa mwendo huu tuuonavyo, basi Otile huenda amejishindia fundo ambalo wengi wamekua wakilitamani kwa kulimeezea mate.

Hiki ndicho kizungu mkuti ambacho kimewaacha wengi wakiwa vinywa wazi huku penzi lao vile linavyozidi kunawiri ndivyo mashabiki wanavyozidi kufurahia ila kwa upande mwingine kuna kundi flani la mashabiki linalopinga mahusiano yao.

Otile kwa upande wake amekua akimtetea Vera Sidika kila anapohojiwa na media tofauti tofauti na mara zote amekuwa akitanguliza penzi lao mbele kwanza. Katika mahojiano na Willy M Tuva kupitia Citizen TV, Otile alisema;

”Vera ni mwanadada genius, nampenda kwakuwa ana IQ ya juu sana, tena ana moyo wa huruma sana, unaweza fikiria Vera Sidika hulia kama amekosewa. Watu wanapenda kujaji watu vibaya ila yeye pia ni binadamu na anahitaji second chance,” alieleza.

Mapenzi yao pia yanazidi shamiri huku si YouTube, Instagram, snapchat na mitandao mingine ya kijamii ikishamiri mahaba yao.

Wekeend iliyopita wawili hao waliwagusa kwa hisia mashabiki wao baada ya kupost picha zikiwaonyesha wakipeana mabusu mazito, wakati huo Vera alikua kavaa gauni jeusi huku akipachika ujauzito bandia kitu ambacho kumewachefua mashabiki na kuwafurahisha baadhi.

Penzi hili ambalo linazidi kushamiri kila siku, limemletea mafanikio makubwa Otile Brown katika muziki wake. Video yake mpya aliyomshirikisha Sanaipei Tande ‘Chaguo La Moyo’ imefikisha views milioni 1.4 katika mtandao wa YouTube ndani ya mwezi mmoja na kuwa video yake ya kwanza kufikia mafanikio hayo.

Imeandikwa na Changez Ndzai kutoka Kenya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents