Bongo Movie

Video: Wasouth wamwalika director wa Bongo aliyetengeneza ‘anaconda’ kwenye movie

Director mkongwe wa filamu nchini, Jully Tax aliyetengeneza nyoka aina ya anaconda kwenye filamu ya ‘Saradini’ amealikwa nchini Afrika Kusini kutengeneza kitu kama hicho.

Juli Tax akikabidhiwa tuzo na Kenneny
Jully ni miongoni mwa wasanii waliopokoa tuzo za kifamilia za H.Baba Jumamosi iliyopita

Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni, Jully Tax amesema kuwa ni watu wachache kwenye filamu zilizofanyika barani Afrika walioweza kufanya hivyo.

“Nataka niseme mbele ya waandishi wa habari kwamba kama nasema uongo wajaribu kuangalia tu, hakuna mwaafrika yeyote amefanikiwa kutengeza nyoka anayefanana na Anaconda ambayo nilihojiwa South Africa ‘Watanzania mnaweza’ nikasema ‘tunaweza’, akasema ‘Afrika kitu hicho hakipo’. Sasa mimi nimetengeneza nyoka kama Anaconda lakini nilibishiwa kabisa Afrika hatuwezi kufanya kitu kama hicho, sisi hatuna mitambo, hatuna vifaa, mimi nikawaambia ‘tayari nimefanya’ na wao wakaniambia ‘umewezaje au wewe mchawi’. Sasa hivi ninaposema hivi mwezi wa kwanza ndio nimeitwa kule natakiwa niende. Nitaiongelea nchi yangu ninakotoka na nitaongelea tuliambiwa Afrika hatuwezi sasa nimeweza hiyo picha hipo tayari na watu wengi sana wametoa comment zao kwamba Tanzania tumeweza kufika hatua fulani,” alisema Jully Tax.

Kitazame kipache kifupi cha video kinachoonesha nyoka huyo kwenye filamu ya Jully Tax.

Pia muongozaji huyo alisema anasikitishwa na pale anapotengeneza filamu nzuri ili ziifikishe Tanzania mbali lakini zinafungiwa kutokana na madai kuwa zinatisha.

“Nilikuwa naumia ndugu zangu, watangazaji wakikaa kwenye media wanasema, ‘sisi watanzania tutafika mbali lini? Kufanya kama wazungu, kufanya kama Nigeria. Unakuta mzungu anamkata mtu kweli mkono, aamkata utumbo kweli. Watanzania hatuwezi, mtangazaji anatangaza hivyo. Sasa tumekuja kuweza picha zinafungiwa. Sasa sijui walikuwa wanaongea kitu gani? Tumeweza kufanya na picha zimefungiwa! Sasa mnataka tufike mbali au? Nina filamu tatu zimefungiwa. Nilitengeneza Zombi, nimeambiwa inatisha sana, na tulikuwa tunaambiwa hatuwezi. Mimi napata uchungu nalia kwanini hatuwezi? Na nimeenda nje nikaambiwa hatuwezi kutengeneza Anaconda na nikatengezeza, sasa nahisi na hii itafungiwa sasa si nitalala njaa? Nahisi hii itafungiwa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents