Burudani

Video ya Lady Jaydee ‘Give Me Love’ nayo yaingia kwenye Top 10 chart ya MTV Base

Msanii mwingine wa Tanzania, Lady Jaydee ameongezeka kwenye orodha ya wasanii wa Tanzania ambao video zao zimeingia kwenye chart za vituo vikubwa vya TV vya kimataifa.

jide mtv

Wiki iliyopita baada ya video ya Joh Makini ‘Nusu Nusu’ kushika namba 1 kwenye chart ya video za wasanii wa Afrika ya MTV Base, na Diamond kukamata nafasi ya kwanza kwenye chart ya Trace Urban, mwanamuziki wa kike Lady Jay Dee pia ameingia kwenye orodha hiyo.

Video ya Jide ‘Give Me Love’ aliyowashirikisha wasanii wa Afrika Kusini, Uhuru, Mazet na Maphorisa, imeingia na kukamata nafasi ya 5 kwenye Official African Chart ya MTV Base wiki hii, huku Joh Makini akishuka kwa nafasi moja hadi nafasi ya pili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents