Michezo

Video ya Pogba akimdhihaki Mourinho yazua ngumzo mitandaoni

Video ya Pogba akimdhihaki Mourinho yazua ngumzo mitandaoni

Mashabiki wa klabu ya Manchester United wameonyesha kuchukizwa na kitendo cha kiungo wa klabu hiyo Paul Pogba kupost video inayoonesha kufurahishwa na kitendo cha kalbu yake kupoteza katika mchezo wao wa Carabao cup dhidi ya Derby Country katika dimba la nyumbani Old Traffo.

Mchezaji huyo alionekana akiwa na furaha sana kwani hakupangwa katika mchezo huo akiwa na wenzake Luke Shaw pamoja na Pereira,

Yote haya yanakuja baada ya kocha wa timu hiyo Mreno Jose Mourinho kusema kuwa nafasi aliyompa Pogba kama kapteni msaidizi na sasa nafasi hiyo ananyang’anya kabisa na hataki tena Mfaransa huyo anae beji ya ukapteni katika klabu hiyo.

Hasira za Mourinho zinaonekana kujaa baada ya Pogba kuongea wakati akiongea na sky sport na kusema kuwa “klabu hiyo inatakiwa kushambulia ikiwa nyumbani sio kucheza kwa kulinda tu,vilabu vingi huiogopa Manchester ikiwa inashambulia zaidi”

Baada ya Pogba kuongea hayo wadau wengi wa soka wamedai kama Pogba anaudhihaki mfumo wa kocha wake wa kulinda zaidi,Pogba baada ya kuulizwa kwanini hawashambulii alisema ” Mimi sijui kwa kuwa mimi sio kocha basi muulizeni yeye”

Jana usiku Pogba alipost Video kwenye akaunti yake ya Instagram akioneshwa kufurahishwa na matokeo hayo ya timu yake baada ya kupoteza katika mchezo huo nyumbani.hadi dakika 90 zinamalizika matokeo yalikuwa 2-2 na waliweza kuingia kwenye mikwaju ya penati na United kupigwa kwa jumla ya penati 8-7 na klabu inayonolewa na mchezaji wa zamani wa Chelsea Frank Lampad.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents