Burudani

Video/Picha: Tazama uzinduzi wa msimu mpya wa show ya The Playlist Times FM

Tarehe 14 January 2017 ulifayika uzinduzi wa msimu mpya wa show ya The Playlist uliokuwa na sura za mastaa kibao waliowahi kusikika kwenye show hiyo misimu iliyopita.

Lil Ommy, Haitham, MC Pilipili na Mansu Li

Show ilikuwa LiVE kwenye redio ndani ya studio za 100.5 Times FM chini ya Presenter wake Lil Ommy huku baadhi ya mastaa wakijiachia kwa VIP treatment na Cocktail na Snacks wakati show inaenda hewani.

Watu walikunywa na kula

Ilikuwa ni meet and great kind a thing na unyama wa kibabe ambao uliuzindua Msimu Mpya kwa mwaka huu Lil Ommy ameuita ‘Toboa Kiburudani’ lengo likiwa ni kumfanya kila kijana anayeamini katika ndoto zake kwenye burudani atoboe.

Romy Jons akiwa na DJ Ally B

Show ilianza kwa wimbo wa kwanza wa Joh Makini – Najiona Mimi kwa lengo la ku inspire na kuhamasisha vijana kupitia burudani.

Show ya The Playlist inaruka kila Jumamosi kuanzia Saa 6 hadi Saa 8 mchana kupitia 100.5 Times FM na Presenter mnyamwezi Lil Ommy.

THE PLAYLIST imekuwa moja ya show kali za burudani kwa vijana inayoongoza kwa kusikilizwa Weekend, ni show ambayo inawashusha mastaa kibao kuchagua ngoma 5 wanazozikubali na kupiga nao mastori kibao kuhusu muziki, fashion na maisha yao kwa pande zote.

Romy Jons akiwa na Amber Lulu

Kwenye show ya The Playlist unapata kuwasikia mastaa wakijiachia kwa muda mrefu zaidi kuzungumzia ishu zote zinazowahusu huku wakitaja list ya ngoma 5 wanazopenda. Utofauti mkubwa wa show hii ni ubunifu na ujanja wa maswali ambayo mastaa wanakutana nayo kwenye show hiyo kutoka kwa Presenter mkali Lil Ommy, The Baddest Boi aka Tambweeeeee.

Mtangazaji wa The Playlist, Lil Ommy
Rapper Baghdad akihojiwa
Miongoni mwa mashabiki wakubwa wa kipindi cha The Playlist
Wanyamwezi walitupia mitupio ya kufa mtu
Romy Jons na Lil Ommy
Lil Ommy na MC Pilipili
Lil Ommy akiwa na wasanii wa MJ Records

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents