Habari

Vipande 15 vya meno ya Tembo vyakamatwa

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na akari wa TANAPA walishirikiana kufanya msako katika pori la hifadhi ya Taifa ya Ruaha lililipo Wilaya ya Mbarali, Mkoani humo walifanikiwa kukamata Pikipiki 06 ambapo baada ya kukaguliwa zilikutwa na Nyara za Serikali ambazo ni Ngozi moja ya Simba na vipande 15 vya meno ya Tembo.

Jeshi la Polisi kupitia taarifa yake iliyoitoa jana kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa, Julai, 27 mwaka huu majira ya saa 16:00 jioni, Jeshi la hilo kwa kushirikiana na askari wa TANAPA walifanya msako huko katika Pori la hifadhi ya Taifa la Ruaha lililopo Kijiji na Kata ya Nyamlala, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya, walifanikiwa kukamata Pikipiki 06 ambazo wahusika wake walikimbia na kuzitelekeza.

Katika Pikipiki hizo, mbili zilikuwa hazina plate namba na nyingine zilikuwa na za usajili MC 386 BHW aina ya Kinglion, MC T.799 CTW aina ya T-Better, MC 755 ADJ, T.461 BZE.

Hata hivyo baada ya kukaguliwa zilikutwa na Nyara za Serikali ambazo ni Ngozi moja ya Simba na vipande 15 vya meno ya Tembo. Upelelezi na ufuatiliaji unaendelea ili kuwabaini na kuwakamata wahusika wa tukio hili.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents