Michezo

Vitendo vya kibaguzi vyazidi kuitia doa Urusi kombe la dunia, FIFA kuja na jibu zito

Shirikisho la soka duniani (FIFA) limefungua uchunguzi dhidi ya wandaaji wa kombe la duniani mwaka huu nchi ya Urusi kufuatia mashabiki wake kutoa kauli za kibaguzi na kichochezi kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa akiwemo kiungo wao Paul Pogba.

Mwandishi mmoja aliyekuwa ndani ya uwanja wa St. Petersburg wakati wa mchezo huo wa kirafiki kati ya Ufaransa iliyo chomoza na ushindi wa mabao 3 – 1 dhidi ya Urusi amesema kuwa alisikia kelele za mashabiki zikiimba nyimbo zinazo husiana na mnyama tumbiri.

Bodi inayosimamia michezo ya kombe la dunia hapo jana siku ya Jumatano imesema kuwa inakusanya vithibitisho vyote vitakavyoweza kuisaidia FIFA katika uchunguzi wake na kuja na majibu ambayo yatakuwa muarubaini wa tatizo hilo.

Hiki nikiwanja cha Luzhniki chenye uwezo wa kuingiza watu 81,006

Hiki ni kiwanja kitakachotumika kwa michezo ya makundi manne ukiwemo ule wa ufunguzi na mmoja wa nusu fainali

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents