Uncategorized

Waandamanaji Sudan walitaka jeshi lijiunge nao kuunda serikali ya mpito

Kundi la wanaharakati wa Sudan wanaoandamana kwa miezi kadhaa sasa dhidi ya Rais Omar al Bashir wamelitolea wito jeshi lizungumze ana kwa ana pamoja nao kuhusu uwezekano wa kuunda serikali ya mpito.

“Tunavitolea wito vikosi vya wanajeshi vizungumze moja kwa moja na muungano kwa ajili ya uhuru na mageuzi ili kurahisisha utaratibu wa amani wa kuundwa serikai ya mpito” amesema Omar el-Digeir, mwanachama wa ngazi ya juu wa kundi hilo, katika taarifa yake nje ya makao makuu ya jeshi wanakopiga kambi tangu Jumamosi iliyopita.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Deutsche Welle, El Digeir amesema wameunda baraza la kuhimiza mazungumzo pamoja na vikosi vya usalama na jumuia ya kimataifa kwa lengo la kukubaliana kuhusu kipindi cha mpito kitakachokabidhi uongozi kwa serikali ya mpito na kukidhi matakwa ya mapinduzi.

“Waandamanaji wamemtaka Rais Omar al Bashir na serikali yake wajiuzulu na kuvitolea wito vikosi vya wanajeshi viache kuiunga mkono serikali wanayosema imepoteza uhalali.

Muungano kwa ajili ya uhuru na mageuzi unawaleta pamoja viongozi wa vyama vya kisiasa, vyama vinavyopigania masilahi ya madaktari, wahandisi na waalimu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents