Siasa

Wabunge watoa milioni 200 kwenda kwa wafiwa Arusha

Leo mapema Bungeni, Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekubaliana kwa kauli moja kuwa posho za kila mbunge kwa siku ya leo zipelekwe kwa wazazi wa wanafunzi waliofariki kwa ajali ya basi la Shule ya awali na Msingi ya Lucky Vincent. Kiasi hicho pamoja na mchango wa speaker, umefikia kiasi cha Milioni 200.

Image result for WABUNGE
               Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,Pia anatarajiwa kuungana na waombolezaji mbalimbali kuaga miili 35 ya marehemu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Hata hivyo licha ya wabunge kutoa rambi rambi hizo Serikali wiki iliyopita ilitangaza kugharamia gharama zote za mazishi ya vifo hivyo.

By Godfrey Mgallah

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents