Habari

Wanafunzi wafunga barabara

Baadhi ya wazazi na wanafunzi mchana huu wamefunga barabara kwa kuweka magogo maeneo ya mtongani kunduchi. Haya yametokea baada ya wanafunzi watatu kugongwa na gari kwenye barabara hiyo na kusababisha foleni kubwa na magari kutopita.Baadhi ya magari yaendayo bahari beach kupitia njia ya tegeta yamejikuta yakikwama njiani kutokana na tukio hilo.

Wazazi,wanafunzi na wakereketwa pamoja na kuweka magogo walitaka kuongezea matuta zaidi katika eneo hilo. Jeshi la polisi lilifika mapema zaidi kutuliza fujo hizo kubwa zilizotokea kwa kurusha mabomu ya machozi.

Mpaka Bongo5 inakwenda mitambo haikuweza kugundua hali ya wanafunzi hao iko vipi na gari liliweza kupatikana. Tutazidi kufuatilia tukio hili na kukuhabarisha zaidi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents