Bongo Movie

Wasanii wa Comedy, wacharuka

1Wasanii_wakiwa_kwenye_kikao

Wasanii wa kuchekesha maarufu kama ‘Macomedy’, wamecharuka na kusema umefika wakati wa kutambuliwa mchango wao katika filamu za Tanzania. akiongea Mwenyekiti wa muda Haji Salum ‘Mboto’ alisema w Wachekeshaji wamekuwa wakidharaulika sana, kwani hata wanapoitwa katika kufanya kipande cha filamu hulipwa ujira mdogo, kuliko hata wasanii wengine wanaoigiza  ‘sliasi’. Wamesema kuanzia sasa

 

hoja_zikitolewa

hawatakubali kuigiza kwa kiasi cha shilingi 15,000, wala 20000 kama walivyozoea kubuluzwa. Pia walisema wasambazaji lazima wawe na usawa, kwani wengi wao wamekuwa wakishindikizwa na wasanii wakubwa, kwamba wachukue filamu zao kwa fedha ndogo jambo linalowapelekea wachekeshaji waendelee kuwa maskini. Alisema mfano mzuri, filamu ya vichekesho ya Uncle JJ, fedha iliyouzwa ni sawa na fedha za filamu 18, za wasanii wa vichekesho, wakati hazina utofauti sana.

kikao_kikiendelea

Pia alisema wasambazaji wamekuwa wakiwahitaji wasanii, lakini wakifika kwenye biashara wao ndiyo huchagua fedha za kuwalipa. Pia Mwenyekiti wa chama hicho, ambacho kipo ndani ya chama cha Shirikisho la Wasanii Tanzania, anasema Wasanii wa vichekesho umefika kipindi wajiheshimu na kama hawapo sehemu ya kazi, au

sehemu ambayo haiwaruhusu kuchekesha, basi wasichekeshe kwani kuchekesha kila sehemu ni sawa na kujidhalilisha.

wasanii_kwa_pamoja
(Wasanii wa kuchekesha wakisikiliza kwa makini katika kikao walichokifanya Vijana)

Matumaini
(Msanii wa vichekesho, Matumaini akifuatilia kwa umakini)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents