![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2016/03/12826165_764330753700260_1108065405_n.jpg)
Mwaka huu nimebadilisha kidogo mtindo wa kuandaa orodha yangu ya kila mwaka ya wasanii wa kuwaangalia katika mwaka husika. Awali nilikuwa naandika orodha nzima na kuwaelezea wasanii wote. Sasa hivi nitakuwa nafanya interview na mmoja mmoja ili watu waweze kumfahamu zaidi. Na anayetungulia ni Layla aka The Voice Fairy. Ameachia kazi yake mpya ‘Hoi Hoi’ hivi karibuni. Mfahamu zaidi hapo chini.