Habari

Watanzania 500,000 wagonjwa wa akili

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amesema Watanzania 500,000 sawa na asilimia moja wana ugonjwa wa akili.

Naibu Waziri amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Morogoro Kusini (CCM), Prosper Mbena aliyetaka kujua ni kwa nini Serikali haina utaratibu wa kuchukua wagonjwa wa akili walio mitaani.

Dkt. Ndugulile amesema kati ya kadirio la wagonjwa 500,000 ni asilimia 48  ndio wanafika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, asilimia 24 wanapelekwa kwa waganga wa kienyeji, asilimia iliyobaiki wanaplekwa katika huduma za kiroho na hao wengine wanabaki mtaani.

Pia ameongeza  kuwa Serikali haina uhaba wa dawa muhimu kwani bajeti imeongezwa. Pia amekazia kuwa Matibabu ya wazee wasiojiweza yanatolewa bure

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents