Habari

Wateja wa GSM kujishindia safari ya Disney Hong Kong (Video)

Kuelekea msimu wa sikukuu maduka ya GSM wanakuletea ofa maalum itakayowawezesha wateja wake kushinda safari ya kuelekea Disney, Hong Kong nchini China.

Akiongea wiki hii jijini Dar es Salaam Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM Farida Rubanza ameeleza kuwa mteja akifanya manunuzi yatakayofikia kiasi cha shilingi laki moja na nusu (150,000) ataingizwa katika droo maalum itakoyomuwezesha kushinda safari ya kuelekea Disney, Hong Kong China.

“Endapo mteja wetu atafanya manunuzi ya kuanzia laki na nusu atafanikiwa kuingia katika droo maalum ambapo mwanzo mwa mwezi January atangazwa mshindi ambaye atapata fursa ya kusafiri Disney, Hong Kong, China” Alisema Farida.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents