Habari

Watu Milioni 32 sawa na asilimia 53 ya watanzania wakamilisha chanjo dhidi ya Uviko-19

WIZARA ya Afya imesema kuwa hadi kufikia Desemba mwaka jana jumla ya watu Milioni 32.5 ambao ni sawa na asilimia 53 ya watanzania wote wamekamilisha chanjo dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19.

Hayo yalibainishwa hivi karibuni na Mchumi Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Afya, Dk. France Lasway wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika mkutano uliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) kuhusu utengaji wa bajeti ya kujiandaa kupambana na magonjwa ya milipuko ikiwemo Uviko 19 na kipindupindu.

Lasway amesema katika kipindi hicho jumla ya dozi Milioni 46.8 za chanjo dhidi ya Uviko-19 zilikuwa zimepokelewa na kusambazwa ambapo dozi Milioni 39.1 sawa na asilimia 84 zimetumika hadi sasa.

“Katika uimarishaji wa huduma za chanjo wizara imeratibu upatikanaji wa chanjo hizo za Uviko -19 kupitia mpango wa kidunia kuhakikisha nchi zinapata chanjo hiyo na misaada kutoka nchi rafiki,” amesema

Hata hivyo amesema wizara kwa kutambua umuhimu wa utayari wa kukabiliana na magonjwa ya milipuko nay a kuambukiza itaendelea kuimarisha huduma za kinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza ikiwemo kuimarisha huduma za chanjo, elimu ya afya kwa umma na huduma za afya ngazi ya jamii.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents