Habari

Wawekezaji wa nje waanza kumiminika Tanzania

Katika siku za hivi karibuni Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikiweka nguvu kubwa kuvitia uwekezaji natakwimu zinaonyesha kuwa jitihada hizo zimezaa matunda kwa kuwa na idadi kubwa ya wawekezaji kutoka nje walioonyesha nia ya kuwekeza hapa nchini.

Vipawa Management Group (VMG) yafanikisha mkutano wa kibiashara kati ya China Council for the Promotion of International Trade (CCPIT- Shenzhen) na Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji wa Mauzo ya Nje (EPZA)

Wakati juhudi hizo zikiendelea hivi karibuni kampuniya Vipawa Management Group (VMG) ilifanikisha mkutano wa kibiashara wa aina yake kati ya wawekezaji wa China Council for the Promotion of International Trade Shenzhen (CCPIT) na Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji wa Mauzo ya Nje (EPZA).

Mkutano huo ulilenga kuchangiza biashara namahusiano ya kibisahara kati ya China na Tanzania. Watu wa China walitaka kupata uelewa wa kina na kuimarisha urafiki katika ya mataifa haya mawilikatika muktadha wa kisheria na sera za serikali.

Katika mkutano huo uliofanyika Agosti 31, 2021 jijiniDar es Salaam China Council for the Promotion of International Trade Shenzhen (CCPIT Shenzhen) walikuwa wanashauku ya kujua fursa zilizopo katikasekta ya kilimo, madini, utalii biashara na viwanda na namna gani Serikali ya Tanzania inaunga mkonouwekezaji.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji wa Mauzo ya Nje ( EPZA) Bw. John Mnali alishiriki mkutano huo wa kibiashara uliofanyikakwa njia ya mtandao ambapo aliwapatia wawekezaji hao maeleze ya mambo yote waliyotaka kujuasambamba na kuwafafanulia juu ya fursa zilizopo.

Kabla ya kuzitaja na kuzifungua fursa zilizopo katikamaeneo husika Mnali alieleza kuwa kwa hapa nchinimwekezaji ana milango mitatu ya kuanzisha uwekezaji wake akiitaja kuwa ni;Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji wa Mauzo ya Nje (EPZA) ambayoinahusisha uwekezaji wa viwanda zinavyozalishabidhaa za kuuza nje, Kituo Cha Uwekezaji- (TIC), Zanzibar Investment Promotion Authority (ZPA), ambayo inasimamia uwekezaji Tanzania-Zanzibar.

Bw. Mnali alieleza kuwa kwa upande wa EPZA mwekezaji mwenyewe anaweza kwa kutumia leseni ya maeneo ya uzalishaji kwa mauzo ya nje- EPZ, aambapo mwekezaji anatakiwa kuuza nje ya nchiasilimia kuanzia 80 ya kile anachokizalisha.

Kuhusu fursa zilizopo nchini katika sekta ya kilimo, Bw. Mnali alisema “Kwa sasa mwelekeo wa Serikali nikupata wawekezaji wa kuongeza thamani katika mazaombalimbali ya kilimo na sio kuuza nje ya nchi yakiwaghafi, pia alieleza kua Kuna fursa kubwa ya kuzalishamafuta ya kupikia kutoka katika mazao yetu”. Kwakuasoko la mafuta ya kula bado ni kuwa ndani na nje ya nchi, na Tanzania inazalisha kwa wingi mazao kama; ufuta, alizeti, na michikichi ambayo ni malighafi ya kuzalishia mafuta ya kula.

Mbali na ukamuaji wa mafuta, Bw.Mnali alieleza kuwa kuna fursa ya kilimo cha maparachichi ambayoyanahitajika kwa wingi katika maeneo mbalimbaliDuniani, sanjari na mazao mengine ya bustanini(horticulture).

Alisema kuongeza thamani sio tu kwenye mazao ya kilimo bali kila sekta ya uzalishaji ikiwa ni pamoja na madini kwa kuyaongezea thamani hapa nchini na siokuyauza yakiwa ghafiTunahitaji vitu kamauchenjuaji, ili kuchenjua na kuyaongezea thamanimadini yetu”.

Katika sekta ya madini ambayo huchangia sehemukubwa ya uchumi wa Tanzania. Bw. Mnali aliongezapia kuna fursa zingine za biashara zilizo wazi kamafursa ya kujenga hoteli za hadhi tofauti tofauti pamojana miundombinu ya burudani na ukarimu kwa watalii.

Katika biashara na viwanda Bw.Mnali alisema kunamengi ya kufanya katika viwanda kwakuwa bidhaanyingi za viwandani Tanzania zinazinunua kutoka nje ya nchi hususani vyakula, dawa na vifaa tiba.

Alisema kwa sasa Tanzania inatumia fedha nyingikununua bidhaa hizo nje ya nchi akitolea mfano wa dawa na vifaa tiba akisema soko lake hapa nchini nikubwa pia aliongezea kwa kusema, taasisi ya kununuana kusambaza dawa (MSD), imepewa idhini ya kusambaza dawa katika nchi za SADC, hivyomwekezaji yeyote katika eneo hilo atakuwa na uhakikawa soko la bidhaa zake.

Mbali na fursa hizo Bw. Mnali alisema, katika sektandogo ya mbao na bidhaa za mbao fursa ni kubwa kutokana na uwepo wa misitu ya asili na miti ya kupandwa, lakini pia kuna fursa ya uvuvi katikamaziwa na eneo la bahari na fursa zote hizo ziko wazikwa wawekezaji.

Vilevile Bw.Mnali alisema kuna fursa ya kuzalishabidhaa za kielektroniki hapa nchini pamoja nauunganishaji wa magari, mashine na mitambombalimbali ambayo inahitaji katika soko la ndani na nje.

Baada ya kusikia fursa hizo CCPIT Shenzhen, ilielezakufurahishwa na uwepo wa fursa hizo na motishaambazo nchi inatoa kwa wawekezaji; hivyo wakaahidikua wawekezaji kutoka China watakuja siku zijazo, hata hivyo walisema Tanzania inafahamika nchiniChina kwa uwepo wa mlima mrefu barani Afrika(Kilimanjaro), Visiwa vya Zanzibar na fukwe nzuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents