Habari

Waziri Mkuu: Magazeti manne yaliyofungiwa yatarudi hewni, hakuna Tv wala Redio iliyofungiwa mpaka sasa isipokua Online TV moja (+ Video)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania @kassim_m_majaliwa amesema hadi sasa Magazeti ambayo yamefungiwa kisheria Nchini Tanzania ni manne ambayo ni Mawio, Mseto, Mwanahalisi na Tanzania Daima ambapo hatua kadhaa zinaendelea ndani ya Serikali ili kuyafungulia magazeti hayo.

“Ninachofurahi ni kwamba hadi leo hii hakuna Redio hata moja au TV iliyofungiwa isipokua Online TV moja, Radio ni moja ilikua Wasafi FM wakati fulani lakini tukawaambia wafanye mapitio na sasa inaendelea na kazi, Magazeti manne yaliyofungiwa hatua zinaendelea ili warejee kwenye uandishi wao, kwa kuwa yalifungiwa kwa mujibu wa sheria basi sheria zilezile zitafata utaratibu wake kwa maelekezo ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, hiyo ndio nia nzuri, nia njema ya Serikali yetu”

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.youtube.com/watch?v=nA6SE8D_iII&t=2s

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents