Habari

Waziri Nchemba amaliza mgogoro wa ardhi uliodumu miaka 9

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefanikiwa kumaliza mgogoro wa ardhi ambao umedumu kwa miaka zaidi ya tisa ambao ulifikia hadi kuhatarisha amani ya kijiji cha Hurui katika kata kikole jimbo la kondoa vijijini wilaya ya kondoa mkoa wa Dodoma.

Mgogoro huo ambao umesababishwa na baadhi ya watu ambao si wajumbe wa kijiji kuuza eneo la kijiji la malisho mwaka 2009 bila mkutano wa kijiji kushirikishwa na kusababisha hali ya sitofahamu mpaka leo. Jitihada za wananchi kutafuta haki ya eneo hilo kwa njia za kisheria hazikuzaa matunda kwani walishindwa katika kesi zote mbili walizofungua katika Mahakama ya ardhi ya wilaya na mkoa hali iliyopelekea sasa mbunge wa jimbo la kondoa vijijini Dr Ashatu Kijaji kumwita waziri wa mambo ya ndani kusaidia kutuliza taharuki hiyo.

Waziri Dr Mwigulu Nchemba baada ya kusikiliza pande zote za kijiji na serikali ya wilaya ameagiza eneo hilo liendelee kutumika kama lilivyopangwa tangu mwaka 1972 kuwa eneo la malisho, amewataka wananchi na viongozi wa vijiji waache kuuza maeneo kinyemela kwani ndio chanzo kikubwa cha migogoro ya ardhi katika vijiji nchini.

Naye mbunge wa jimbo la kondoa vijijini ambaye pia ni Naibu waziri wa fedha Dr ashatu kijaji amesema amechoka na migogoro ya ardhi katika jimbo lake,yule ambaye atawafikisha katika migogoro watashughulika naye kwa sheria na taratibu za nchi.

Aidha Dr Ashatu amesema kuwa kwasasa hawawezi fanya shughuli za maendeleo katika baadhi ya vijiji kama kujenga madarasa na miundombinu ya maji na umeme kwasababu ya migogoro ya ardhi iliyopo hivyo kwasasa migogoro basi ili wafanye kazi huku akimshukuru Mkuu wa wilaya kwa jitihada kubwa zakusaidia kumaliza migogoro hiyo anayoonyesha

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Hurui Ramadhani Selemani amesema migogoro hiyo imeletwa na baadhi ya wajumbe wa serikali ya vijiji waliopita kwa kuuza maeneo zaidi ya ekari 52 ya malisho bila kushirikisha mkutano wa kijiji hali ambayo imeleta mgogoro mkubwa na kuhatarisha amani ndani ya kijiji.

Wananchi wa kata ya kikole wamemshukuru waziri wa mambo ya Ndani ya nchi kwa kuwarudishia maeneo yao kwani kwasasa amani itarudi tena katika kata yao na maendeleo yatakuja kwani watafanya shughuli kwa amani

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents