Siasa

Waziri wa afya atimuliwa baada ya vifo vya watoto 11 ajali ya moto Senegal

Rais Macky Sall wa Senegal amemwachisha kazi waziri wake wa afya Abdoulaye Diouf Sarr baada ya vifo vya watoto wachanga 11 vilivyosababishwa na ajali ya moto kwenye hospitali ya uzazi.

Ni watoto watatu tu walioweza kuokolewa katika ajali hiyo iliyosababishwa na hitalafu ya waya wa umeme. Waziri wa mambo ya ndani wa Senegal amesema uchunguzi utafanyika juu ya mazingira ya hospitali hiyo na sehemu nyingine zinazotoa huduma za afya.

Maafa hayo ya moto yalitokea kwenye hospitali ya mji uliopo umbali wa kilometa 120 kutoka mji mkuu wa Senegal, Dakar.

Mwaka uliopita watoto wachanga wanne pia walikufa baada ya moto kuzuka kwenye hospitali nyingine iliyoko kaskazini mwa Senegal. Rais Macky Sall amemteua waziri mwengine mpya wa afya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents