Uncategorized

Waziri wa usalama wa ndani wa Marekani ajiuzulu

Waziri wa usalama wa ndani wa Marekani Kirstjen Nielsen amejiuzulu jana, kutokana na kile alikiona kuwa ni ukosefu wa uungaji mkono kutoka kwa washirika wa Rais Donald Trump kuhusu idadi ya familia za Kutoka Amerika ya Kati zinazovuka mpaka wa kusini na kuingia nchini humo.

Tokeo la picha la The US Secretary of Homeland Security Kirstjen Nielsen

Lwa mujibu wa shirika la habari la Deutsche Welle (DW), Trump ametangaza jana kwenye mtandao wa Twitter kuwa Kamishna wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka nchini Marekani Kevin McAleenan atachukua nafasi ya kaimu katika wizara huyo.

McAleenan ni afisa wa muda mrefu wa ulinzi wa mipaka ambaye anaheshimiwa sana na wabunge na ndani ya serikali.

Uamuzi wa kumteua afisa mwandamizi wa uhamiaji kuchukua nafasi hiyo ya uwaziri inaonyesha kipaumbele cha Trump kwa ajili ya wizara hiyo kubwa iliyoundwa kupambana na ugaidi kufuatia mashambulizi ya Septemba 11.

Tokeo la picha la The US Secretary of Homeland Security Kirstjen Nielsen

Nielsen alisafiri pamoja na Trump Ijumaa iliyopita kwenda kwenye mpaka wa Marekani na Mexico kushiriki katika mazungumzo na maafisa wa mpakani na polisi wa eneo hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents