Burudani

Wimbo wa Fever wa Wizkid wavunja rekodi hii Nigeria kupitia mtandao wa VEVO

Video ya wimbo wa Fever wa Wizkid wavunja rekodi hii Nigeria kupitia mtandao wa VEVO

Msanii wa muziki kutoka Nigeria Ayodeji Ibrahim Balogun anayejulikana kwa jina la kiusanii kama Wizkid amefanikiwa kuvunja rekodi nyingine nchini Nigeria kupitia wimbo wake wa Fever.

Wimbo huo wa Wizkid ambao umeachiwa video ukiwa na siku moja umefanikiwa kuivunja rekodi ya nyimbo yake ya Come Closer aliyomshirikisha msanii kuto Canada Drake ambao ulivunja rekodi kwa kufikisha Views (watazamaji) milioni moja ndani ya masaa 23.

Awamu hii wimbo huo mpya umevunja rekondi ambao haijawahi kutokea nchini Nigeria kwa kufikisha Views milioni moja ndani ya masaa 20.

Wizkid anakuwa msanii wa kwanza kufanya hivyo nchini Nigeria kupitia mtandano wa VEVO kuivunja rekodi hiyo lich ya kuwahi kutokea msanii kutoka Tanzania ambaye ni Alikiba kufanikiwa kufikisha Views milioni mbili ndani ya siku tatu kupitia wimbo wake wa “Seduce me”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents