Michezo

Yanga waidhalilisha Tanzania nchini Kenya, watolewa mapema kwenye michuano ya SportPesa Super Cup 2018

Klabu ya Yanga imekuwa timu ya kwanza kutolewa kwenye mashindano ya SportPesa Super Cup kwa kukubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya klabu ya Kakamega HomeBoys, mchezo uliopigwa mjini Nakuru, Kenya kunako dimba la Afraha.

 

Mabao mawili ya Kakamega yamefungwa na Allan Wanga huku moja likiwekwa kimiani na Opondo. Na goli pekee la Yanga limefungwa na Matheo Anthony kwa njia ya mpira wa adhabu.

Kwa matokeo hayo Kakamega inafuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo yenye jumla ya timu nne kutoka Tanzania ambazo kwa sasa zilizosalia ni JKU, Singida United na Simba SC.

Bingwa wa michuano hii atakutana na Everton kwa hiyo Yanga moja kwa moja wamekosa nafasi adhimu ya kukikupiga na Everton nchini England kunako  dimba la Goodison Park.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents