Michezo

Yaya Toure ashinda tuzo ya BBC na kuweka rekodi mpya

Kiungo wa klabu ya Manchester City ya England na timu ya taifa Ivory Coast Yaya Toure ameshinda tuzo ya mchezaji bora Afrika inayotolewa na Shirika la Utangazaji nchini England (BBC) kwa mwaka 2015.

Toure

Toure anakuwa mchezaji watatu ambae amewahi kuchukua tuzo hiyo mara mbili akiungana na Nwanko Kanu pamoja na Jay-Jay Okocha (wote wa Nigeria) ambao waliwahi kutwaa tuzo hiyo mara mbili.

Nyota huo wa Ivory Coast amesema anajivunia kuwa mshindi wa tuzo hiyo ambayo mshindi hupatikana kwa kupigiwa kura na mashabiki.

‘Najivunia sana. Kupokea tuzo hii kutoka kwa mashabiki siamini’., Toure ameiambia BBC Sport.

Yaya Toure amewashinda Yacine Brahimi (Algeria), Pierre-Emerick Aubameyang (Gagon), Andre Ayew (Ghana) na Sadio Mane (Senegal) ambao walikuwa wakiwania tuzo hiyo kwa mwaka 2015.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents