Burudani

Young Killer ajiunga na kundi la Mtu Chee, achukua nafasi ya Young Dee aliyejitoa

Baada kuwa kimya kwa takribani miaka miwili, Kundi la Mtu Chee lililokuwa linaundwa na rappers watatu, Ibrahim Mandingo a.k.a Country Boy, David Genzi a.k.a Young Dee pamoja na Boniventure Kabogo a.k.a Stamina linarudi rasmi likiwa na mabadiliko.

COUNTRYBOY1
Country Boy

Member na mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo Country Boy amesema kuwa Mtu Chee imepata member mpya ambaye ni Young Killer aliyechukua nafasi ya Young Dee aliyejitoa kwenye kundi.

Akizungumzia sababu za Young Dee kujiondoa Country Boy amesema “Kuna vitu ambavyo vimeingiliana kutokana na kwamba Young Dee amekuwa na majukumu yake na management yake imekuwa kama inampa ugumu kufanya kazi na sisi kwahiyo sisi tumeamua kuendeleza kufanya, tumemuongeza Young Killer.” alsema kupitia Planet Bongo ya EA Radio.

Ameongeza kuwa wanategemea kuachia wimbo mpya wiki ijayo uitwao ‘Mimi’ ambao watakuwa wamemshirikisha Jux na Vanessa Mdee.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents