Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Albamu ya Dj Khaled yashuka chati za Billboard 200

Albamu ya Dj Khaled ‘Grateful’ imeshuka katika chati za Billboard 200, huku nafasi yake ikichukuliwa na kundi la Brand New kupitia albamu yao ya ‘New Science Fiction’.

Kwa mujibu wa chati za Billboard 200 zinaonyesha kuwa albamu ya rapper huyo imeshika nafasi ya saba wakati awali ilikuwa ikishikiria nafasi ya kwanza  kwa wiki mbili mfululizo mwezi Julai.

Grateful ni albamu ya 10 kwa maisha ya muziki kwa msanii huyo ambayo iliingia sokoni Juni 23 mwaka huu na tayari imeshaonyesha mafanikio mbalimbali kupitia ngoma zake tofauti tofauti 23.

Hizi ni albamu kumi za juu katika chati za Billboard 200:-

1. Science Fiction – Brand New
2.Project Baby Two – Kodak Black
3. DAMN. – Kendrick Lamar
4.The Peace And The Panic – Neck Deep
5. Rainbow – Kesha
6. American Teen – Khalid
7. Grateful – DJ Khaled
8. Divide – Ed Sheeran
9. Paranoia: A True Story – Dave East
10. Evolve- Imagine Dragons

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW