Burudani

Justin Timberlake aachia albamu yake ya nne

Baada ya kupita takribani miaka mitano tangu Justin Timberlake alipoachia albamu yake ya ‘The 20/20 Experience’, msanii huyo ameachia albamu yake mpya iitwayo ‘Man Of The Woods’.

Albamu hiyo ina ngoma 16 ambapo pia amewakutanisha wasanii kama Alicia Keys, Chris Stapleton, Danja, Pharrell Williams, na Chad Hugo.

Baadhi ya nyimbo ambazo zinapatikana kwenye nyimbo hizo ni pamoja na ‘Filthy’, ‘Sauce’, ‘Young Man’, ‘Montana’, ‘Wave’, ‘Morning Light’ na nyingine.

Man Of The Woods ambayo ni albamu ya nne ya muimbaji huyo, kwa sasa imeanza kupatikana katika mtandao wa Spotify.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents